NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Korogwe

VITUO vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, ambayo inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97, viko katika hali nzuri, Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S. Mahenda, amesema Leo Desemba 18, 2017.

Hata hivyo amesema, mashine moja kati ya mbili kwenye kituo cha Hale, haifanyi kazi na iko katika matengenezo. “Niwahakikishie tu kwamba matengenezo hayo ambayo bado hayajaanza hayataathiri upatikanaji umeme kwa sababu vyanzo vya umeme vimeongezeka.” Alisema.Akifafanua zaidi Mhandisi Mahenda alisema, New Pangani Falls inazalisha umeme Megawati 68, Hale Megawati 21, na Nyumba ya Mungu Megawati 8 na uwezo wa vituo kutoa umeme wa kutosha.

Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea vituo vya Hale na New Pangani Falls Mhandisi Mahenda, alisema, kituo cha Hale kilijengwa mnamo mwaka 1961 na kuanza kufanya kazi mwaka 1964 na kuwa kituo cha kwanza kabisa cha kuzalisha umeme wa maji katika historia ya nchio yetu. 

“ Utaona umri wa mitambo hiyo ni miaka 53, na moja ya mashine hizo imeharibika na kufanya uwezo wa kituo wa kutoa Megawati 21, kupungua hadi Megawati 8, lakini niwahakikishie wananc hi licha ya upungufu huo, bado TANESCO inao uwezo wa kuzalisha umeme unaohitajika, kwani vyano vya umeme vimeongezeka.” Alisema. 
Mhandisi Mahenda S. Mahenda, Meneja wa Vituo vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, vinavyohusisha inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97
Valvu ya kupitisha maji yanayopelekwa kwenye mashine za kufua umeme, kwenye kituo cha nguvu za umeme cha Hale ikivuja. Mhandsi Mahedna alielezea hali hiyo kuwa haina taathira kubwa na inatokana na mashine hizo kuwa na umri mrefu Zaidi.
Bwawa la maji Pangani Pangani Falls.
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha New Pangani Falls cha 132 kV.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...