Na Bashir
Yakub.
Mara kadhaa
nimezungumzia kuhusu namna
bora na ya
kisheria ya kuuza
na kununua nyumba
au kiwanja kutoka
kwa msimamizi wa mirathi
baada ya mmiliki
halisi kufariki.
Leo tena makala haya
yataeleza kubadili jina kutoka
jina la marehemu
kwenda kwa msimamizi
wa mirathi. Kubadili huku
kunaweza kuwa na
lengo la kuuza, kupangisha , kugawa
kwa warithi au
hata kubadili tu kwa maana
ya kubadili bila
malengo haya juu.
Maelezo katika makala
haya yatatoka Sheria ya Usajili
wa Ardhi sura
ya 334 na kanuni zake za
mwaka 1954, pamoja na Sheria ya
usimamizi wa Mirathi sura ya 352 na kanuni zake
za mwaka 1963.
UTARATIBU NI
HUU.
1.Lazima kwanza ufungue mirathi na
apatikane msimamizi wa
mirathi. Tumeeleza mara
nyingi utaratibu wa kufungua
mirathi . Tulisema kuwa, kwa marehemu
aliyekuwa mkristo utafungua
mahakama maalum ya wilaya(district delegate) au mahakama kuu ,
na kwa marehemu
aliyekuwa muislam au
aliyeishi kimila bila
dini utafungua mahakama
ya mwanzo au
Mahakama kuu.
Kwahiyo hoja hapa ni
kuwa hatua ya
kwanza lazima awepo
msimamizi wa mirathi.
2. Msimamizi wa mirathi
atakapokuwa amepatikana basi
atapewa fomu namba 4 na 5 za usimamizi
wa mirathi. Fomu hizi zinatolewa
na mahakama na
ni uthibitisho kuwa
fulani ni msimamizi
wa mirathi halali. Hoja hapa hakikisha unazo hizo
fomu mkononi.
3. Ukishakuwa na
fomu hizo mkononi
basi utatakiwa kutafuta
na kujaza fomu
nyingine iitwayo fomu ya
uwakilishi maalum wa
marehemu kisheria( Lega personal representative). Fomu hii
ni namba 20 kwenye
kanuni za usajili wa ardhi.
KUSOMA
ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...