Mradi wa majaribio wa miezi 15 wa watoto waliokosa shule, kujifunza wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti umezinduliwa mkoani Tanga.

Mradi huo uliozinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza.

Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika.

Aidha kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na mashirika.

Katika utoaji elimu huo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11 na watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, mkoani Tanga, Juma Killo akitoa salamu kwa XPrize, UNESCO, WFP na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo, Afisa Miradi wa UNESCO, Nadia Marques (wa tatu kushoto), Ofisa Elimu wa wilaya ya Pangani, Mbwana Mohamed (wa tatu kulia), Kaimu Ofisa Elimu Lushoto, Beatus Kipfumo (wa pili kulia) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, Xavery Njovu (kulia).
Mradi huo wa Tanga ambao utagusa watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 vya wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani unatoa changamoto kwa timu ya wabunifu kuwezesha watoto walio na fursa ndogo ya kuingia katika elimu darasani kujifunza stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia tableti wakijifunza wenyewe.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Zenith, Muheza Mkoani Tanga, Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi huo Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaendana na majukumu ya Unesco ya kuhamasisha elimu jumuishi katika kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wakiwemo wa jamii za pembezoni zilizo nyonge zinapata fursa.

Alisema UNESCO inatekeleza majukumu yake kwa kuisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha kutoa elimu bora kwa wananchi wake wote na hata wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu kutokana na mazingira yao au maeneo yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...