Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw.Kheri James mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Chuo Cha Mipango mjini Dodoma wa pili kutoka kulia anayeangalia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita.PICHA NA MICHUZI JR DODOMA.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Rais Dkt Ali Mohamed Shein akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Bi. Tabia Mwita baada ya ushindi wake katikati anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri Denis James akiwa amebebwa na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kutajwa kuwa ndiye Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo kwa miaka mitano
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa UVCCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi katika mkutano huo.

Mara baada ya kutangazwa tu kuwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM),Kher Denis James,kwa furaha kubwa iliyokwenda mpaka kwa Wajumbe wenzake,ilibidi zitumike nguvu za ziada kupunguza vurugu za shangwe zilizotarajiwa kutokea ukumbini hapo,kama uonavyo Mwenyekiti akiwa katika mikono salama ya utuliu akielekezwa kwenda jukwaa kuu.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tisa wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo,ambapo Jumuiya hiyo leo imefanya chaguzi zake za viongozi mbalimbali. 
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita akimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya Bi. Tabia Mwita.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Kassim Majaliwa pichani kushoto akitazama tukio la pongezi kutoka Makamu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake Mh. Mboni Mhita  akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri  James.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...