Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

Kampuni ya fuya Nicol imefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Nicol, Felix Mosha na aliyekuwa Mtendaji Mkuu (CEO, Kathleen Armstrong.

Kesi hiyo ya madai namba 282 ya 2017 inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respius Mwijage, ambapo  upande wa wadaiwa umetakiwa  kupeleka utetezi wao,Desemba 20, 2017 na kesi hiyo imepangwa kutajwa Januari 24,2018.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, upande wa wadai, wanaiomba mahakama hiyo, iamuru wadaiwa hao walipe kiasi cha Sh 180,096,097 kama gharama za hasara walizoingia.

Pia wanaomba mahakama iamuru warejeshe magari, walipe riba ya asilimia 26% pamoja na gharama za kesi.

Katika kesi hiyo, akina Mosha ambao ni wadaiwa wanatetewa na Wakili Hurbet Nyange huku Nicol  ambaye ni mdai anawakilishwa na Wakili Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya uwakili ya BM.

Kwa mujibu wa kesi hiyo inadaiwa kuwa Mosha pamoja na kuondolewa uenyekiti  na wanahisa  mnamo mwaka 2012, lakini bado ameshindwa kukabidhi gari  la ofisi aina ya Landcruiser namba T 133 AVG ambapo ilipelekea ofisi ya Nicol kutafuta usafiri mwingine.

Kwa upande wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Kathleen Armstrong  yeye anadaiwa  kwamba akiwa amesimamishwa  na baada ya kuondolewa  na wanahisa,  alishiriki katika kutapanya mali za Nicol ikiwamo kuuza gari aina ya Mitsubish Center Fuso bila idhini ya bodi ama Wanahisa .

Mahakama imeagiza mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, Kathleen Armstrong ambaye ni raia wa Marekani apelekewe notisi  kwa njia sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...