Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu. 
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke. 
Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou. 
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri, na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa Mambo ya Nje 
Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 
Picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...