Na: Beatrice Lyimo,MAELEZO-DODOMA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameihimiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuharakisha uandaaji wa Sera ya Riba ambayo zitaifanya taasisi za kifedha kuwa na riba zinazowiana na nafuu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa akizundua tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo jengo la LAPF Makole ambalo ni tawi kubwa kwa mkoa wa Dodoma.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mabenki kutolipwa na wakopaji kwa kuanzisha mfumo wa kuhifadhi taarifa za mkopaji ambazo zitawezesha benki zote kuwatambua wakopaji na kuweza kuchukua tahadhari stahiki, pia itaendelea kutoa vitambulishio vya Taifa ambavyo kwa sasa vina taarifa zote muhimu za mwananchi,” amefafanua Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa BOT kudhibiti matumizi ya dola na fedha nyingine za kigeni hapa nchini kutokana na kuharibu uchumi wa nchi. Dkt. Magufuli ametolea mfano wa fedha zilizoshikiliwa Airport ya Dar es Salaam ambazo ni zaidi ya Dola Bilioni Moja zikiwa hazijulikani zilipokuwa zikipelekwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...