Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul amesema taasisi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuendelea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu kuwalinda watoto hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ijumaa katika ziara yake ya siku nne nchini Tanzania, alisisitiza kwamba kupitia SOS Children Village ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuangazia masuala mbalimbali yanayoathiri usalama wa watoto nchini Tanzania.

“Tutaendelea kufanya kazi na jamii pamoja na serikali katika kuweka mazingira mazuri ya baadaye kwa watoto ili kuhakikisha huko mbeleni wanatimiziwa mahitaji yao muhimu,” alisema.

Ziara ya Rais huyo ilianzia Zanzibar ambako alitumia fursa hiyo kutembelea watoto na kukagua baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa na asasi hiyo.

Kwa Dar es Salaam Kaul atakutana na watoto na kukagua miradi michache ambayo inasimamiwa na asasi hiyo pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikalini.
Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul (kulia) akiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. Rais huyo yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa SOS Village Tanzania, Dk. Mary Nagu.
Rais wa SOS Children’s Village, Siddhartha Kaul akisalimiana na wamama waliojitolea kuwalea watoto Shirika hilo baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo jana jijini Dar es salaam. Rais huyo yupo nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo atakagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.
Kikundi cha watoto wanaolelewa katika makazi ya SOS children’s village Ubungo jijini Dar es salaam, kikitoa burudani ya aina yake wakati wa hafla ya kumpokea rais wa Shirika hilo ambaye aliwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 4 mwishoni mwa juma. Raisi wa Shirika hilo ameweza kukagua miradi ya SOS Children’s village na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.
Rais wa SOS Children’s Village Siddhartha Kaul, akisalimiana na watoto wanaolelewa katika kituo cha SOS Children’s village kilichopo Ubungo hivi karibuni jijini Dar es salaam. Rais wa Shirika hilo alitua nchini kwa ziara ya siku 2 ambapo alikagua miradi ya shirika hilo na kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...