Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega jana amekamata samaki aina ya sangara wachanga na wazazi tani 11 waliokuwa wakitoroshwa kwenda nchi jirani ya DRC kwa kukwepa kulipa kodi.

Samaki hao tani 11 walitakiwa kulipiwa ushuru wenye thamani ya Tsh.99,000,000, badala yake wafanyabiashara hao wa kikongo walikwepa kulipa ushuru huo kwa kuchukua kibali kinachoonesha samaki hao wanaenda kuuzwa Tunduru mkoani Ruvuma

Akizungumza na uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe Ulega amesema kuwa watumishi wa serikali watangulize Uzalendo katika nafasi zao wanazozitumikia kuliko kuendekeza rushwa."Jamani naombeni sana msimamieni sheria Ili kulinda Rasilimali zetu zisitoroshwe kwenda nje bila kulipiwa Kodi,tumuunge Mkono Rais wetu John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Rasilimali hizi zinawanufaisha wananchi na sio watu wachache"alisema.

Ulega aliesma ni kinyume cha sheria kuvua samaki wachanga na wazazi, na ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Ilemela kwa kupitia Mkurugenzi wake kuhakikisha wanasimamia sheria ipasavyo na hakuna samaki wachanga na Wazazi kuvuliwa.

"Ikitokea wakati wa ukaguzi wenu mmekamata samaki wachanga au wazazi taifisheni na sheria ichukue mkondo wake kwa yoyote anayehusika au anayevunja sheria kwa kujua au kutokujua"alisema Ulega.Katika hatua nyingine Mhe. Naibu Waziri Abdalla Ulega alipata fursa ya kuhutubia wafanyabishara katika soko hilo,mara nyingi Naibu Waziri alikatishwa hotuba yake kwa kushangiliwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara waliokusanyika sokoni hapo.

Aidha wafanyabiashara hao walimweleza Naibu Waziri changamoto wanazokumbana nazo hapo sokoni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi na salama na ubovu wa miundombinu ya vyoo katika soko hilo.

Mhe.Ulega amempa siku tatu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kuhakikisha maji na miundombinu ya vyoo sokoni hapo inashugulikiwa ndani ya siku tatu."Mkurugenzi nakuagiza kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hili viwe vimepatiwa Ufumbuzi".Alisema Ulega.
 .Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akipima ulefu mmoja wa Samaki waliokamatwa tani 11 wakisafirishwa kinyume na taratibu mkonani katika soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa  Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akifafanua jambo mbele ya watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
 Naibu Waziri wa Mifugo na  Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na wafanya biashara wa katika  soko la Samaki la Kimataifa (Mwaloni-Kirumba) jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akiwa akisalimiana na wafanyabiashara katika soko hilo. Picha  zote  na Emmanuel Massaka,MMG Mwanza.

.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akikagua miundo mbinu ya maji katika soko hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bw.John Wanga kufikia Jumatatu Decemba 18 changamoto ya maji safi na Salama na Miundombinu yote ya vyoo vya soko hilo viwe vimepatiwa Ufumbuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...