NA TIGANYA VINCENT

SERIKALI inatafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa asilimia 30 ya kuziwezesha Kaya Masikini ambazo hazikuweza kuingizwa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ajili ya kuwaondoa kwenye umaskini. Kauli hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Captain (Mstaafu) George Mkuchika wakati wa ziara yake ya kutembelea kaya masikini.

Alisema kuwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa asilimia 100 ya kaya masikini nchini zinafikiwa kuwa na uwezo kupata chakula milo yote mitatu ,, sehemu ya kulala na mavazi. Captain (Mstaafu)  Mkuchika alisema kuwa hadi hivi ni asilimia 70 ya kaya masikini ndio wameshafikiwa na Mpango wa Kunusuru kaya masini unaosimamiwa na TASAF na hivyo kuwa uhakika wa kupata mahitaji muhimu.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania imelenga kuhakikisha kuwa inavifikia vijiji na kaya zote ambazo hazikufikiwa na Mpango wa Kunusuru Kaya masikini. Captain (Mstaafu) Mkuchika alisema kuwa Serikali inaendelea kutafuta fedha ambapo ndani ya mfupi wataweza kuzifikia kaya masikini zilizobaki  ili nao waweze kunufaika na kujinusuru na umaskini.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathaniel Linuma alisema kuwa hadi kufikia Agosti mwaka huu walengwa 39,293 walikuwa walipatiwa kiasi cha bilioni 20  ikiwa ni sehemu ya kuwezesha kaya maskini. Aliongeza kuwa jumla ya shilingi milioni 563 zililipwa kwa walengwa chini miradi ya kutoa ajira za muda kama vile uoteshaji miti, ukarabati wa mabwawa, miradi ya barabara. Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masiki katika Manispaa ya Tabora walisema kuwa mpango huo umesaidia kuwa na uhakika wa watoto wao kuzoma na kula milo mitatu.

Mmoja wa wanufaika hao Cecelia Paulo alisema kuwa kabla ya kuanza kupata fedha za Mpango wa kunusuru kaya masikini alikuwa akitegemea vibarua katika mashamba yake ili aweze kumudu kupata walau mlo moja kwa ajili ya wajukuu wake aliachiwa na mwanae lakini hivi sasa analima katika shmaba lake na kupata chakula cha kutosha. Aliongeza kuwa hivi sasa wajukuu zake wanakwenda Shule bila matatizo kwa kwa sababu anazo fedha za kuwanunua mahitaji ya shule zikiwemo sare, madaftari na vitabu kwa sababu ya fedha ya TASAF.

Naye Hadija Jumanne alisema kuwa fedha za TASAF zimsaidia kuanzisha ufugaji wa bata na kuhudumia watoto wake na kuongeza kuwa hivi sasa hana tena shida ya chakula kama ilivyokuwa kabla ya hapo. Mariam Kaombwe alimweleza kuwa fedha hizo zimeweza kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii na kuanza kuapata matibabu bila shida. Alisema kuwa manufaa mengine ni pamoja na kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya kuuza nyanya, vitunguu na ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya siment.

Mariam aliiomba Serikali iendelea kuwasaidia kupitia TASAF ili wakamilishe miradi yao waliyokwisha kuanzisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...