Na Said Mwishehe wa Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya amesema ipo haja ya kuwa na mkakati maalumu wa kufuatilia viwanda vinavyoanzishwa nchini ili kukomesha vifo vya viwanda.
Manyanya aliyasema hayo wakati wa uhitimishaji wa Maonesho ya  pili  ya bidhaa za viwanda vya ndani yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, amesema kuna idadi kubwa ya viwanda vimeanzishwa nchini, hivyo jukumu lililopo ni kuvisimamia ili viendelee kuwepo.

"Ni wakati muafaka sasa wa kusimamia viwanda vilivyopo nchini vifo vya viwanda vikomeshwe na hii itatoka na ufuatiliaji na usimamizi wa karibu,"anasema.

Mhandisi Manyanya amesema mfumo wa kufuatilia viwanda unawezekana kwani kuna maofisa biashara na wataalamu wengi,hivyo watakuwa na jukumu la kuvisimamia katika  maendeleo yake.

"Kwa lugha rahisi niseme hivi tuwe na zahanati za viwanda kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya ukuaji wa viwanda vyetu,"amesema.

Pia ameonya tabia ya baadhi ya wamiliki wa viwanda kuwa  wadanganyifu kwa Wizara na watakaobainika watachukuliwa hatua.
"Tunazo taarifa kuna wamiliki wa viwanda waliouziwa viwanda na Serikali, wanachokifanya hawazalishi bidhaa na badala yake wanunua kutoka viwanda vya nje na kujifanya wanazalisha hapa nchini,"amesema.
 Naibu Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya akizungumza katika uhitimishaji wa maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda vya ndani katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye viwanda na kampuni mbalimbali walioshiriki maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda vya ndani katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...