Mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amewataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kukiishi kiapo cha utii kwa matendo na si maneno. 

Hayo ameyazungumza leo Disemba 16, 2017 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya mgambo ambayo yalifanyika katika Kata ya Rubeho halmashauri ya wilaya ya Gairo ambapo mgeni rasmi aliwaasa wahitimu kutii yale yote waliyofundishwa ili kujenga uchumi wa Taifa. 

Katika hotuba yake Mhe. Mchembe aliongeza kuwa mgambo wanapaswa kutumia elimu waliyoipata ili kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka bila kuwaonea au kuwatesa wananchi. "Nawaombeni sana ndugu zangu mafunzo mliyoyapata ni muhimu sana katika taifa letu ni vyema sasa na nyie mkayaishi yale yote mliyofundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu mliyoshiriki," alisema Mhe. Mchembe. 

Aliongeza kuwa ni vyema mgambo wakawa mabalozi wema wa amani na si wao wawe mstari wa mbele katika vitendo vya rushwa, unyanyasaji wa wananchi na kuepuka kujihusisha kwenye uharifu kwa kukodisha magwanda yao. Mhe. Mchembe aliwataka viongozi wa wilaya kufanya usaili tena kwa wale mgambo wote ambao wameshapitisha miaka 10 ili waweze kurudi kupata mafunzo zaidi.

"Kazi hii ya mgambo inahitaji kuendelea kujifunza mara kwa mara hivyo nawaomba viongozi wote fanyeni upya usaili wale wote ambao muda wa miaka 10 umepita warudie katika mafunzo waweze kuongeza ujuzi zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride. 
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo. 
Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga akitoa machache mbele ya mgeni rasmi. 
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride. 
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakipita mbele ya mgeni rasmi kwa gwaride la kutoa heshima. Na Kajunason/MMG. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...