Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akishiriki kupanda katika Shule ya Msingi Jeshini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru, huku baadhi ya makamanda, maofisa na wapiganaji wa Jwshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha Anga cha 601 KJ, walimu na wanafunzi wakishuhudia.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi (Base Comender) Kanali Albert Joseph Kitumbo akipanda mti katika maadhimisho ya siku kuu ya Uhuru yaliyofanyika Shule ya Msingi Jeshini.
Mkuu wa Kikosi cha Anga cha 601 KJ cha Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Bryceson Msilu akipanda mti kwa kushirikiana na wanafunzi wa shule wa Shule ya Msingi Jeshini wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru iliyoadhishwa jijini Mwanza kwa kupanda miti.Nyuma ya mkuu huyo wa kikosi ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WANANCHI wa Mkoa wa Mwanza wametakiwa kujenga uzalendo kwa mkoa na taifa lao kwa kufanya kazi na kulinda rasilimali za nchi ziweze kuwanufaisha wao, vizazi vya sasa na vijavyo. Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kwenye Maadhimisho ya Siku yaUhuru iliyoadhimishwa kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Jeshini iliyopo wilayani Ilemela .

“Tujiulize , mimi ni mzalendo kwa jamii na taifa langu ? Kufanya kazi ni uzalendo wa kutosha na unaongeza tija katika kuboresha uwezo, kuitikia na kushiriki shughuli za kijamii na hivyo kila mmoja awajibike kwa kujenga uzalendo kwa mkoa wetu na taifa laetu,”alisema Mongella.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ulinzi wa rasilimali za nchi ili ziweze kunufaisha jamii ni uzalendohoji na kuhoji wananchi wangapi wametimiza wajibu wao kwa kuzilinda rasilimali hizo. Pia aliikumbusha jamii kupanda miti ili kutunza na kulinda mazingira na kuacha kukata miti ovyo, kuchimba mchanga, kupasua mawe na kufanya hivyo mazingira yanaharibika.

“Upandaji miti uwe endelevu na uwe sehemu ya utamaduni wetu, tusisubiri wakati wa sherehe ndio tupande miti.Tukifanya hivi watoto wetu watajua umuhimu wake na wataelewa maana ya misitu na rasilimali za misitu,”alisema Mongella na kushauri kila shule kupanda miti ya matunda ili wanafunzi wafaidike badala ya miti ya mbao pekee.

Akizungumza kwenya sherehe hizo, mwanamazingira wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Envalomental Convertion (TECO) John Masweta alishauri kupanda misitu mikubwa ya miti kwa ajili kumbukumbu ya Uhuru na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na kuiomba serikali ya mkoa kufanya harambee ya kukusanya fedha za kuwezesha upandaji miti wa misitu hiyo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshini Pelesia Manyama aliwataka wananchi wanaoishi jirani na shule hiyo kuacha kuchungia mifugo yao kwenye eneo lililopandwa miti.

Awali Mkuu wa Kikosi cha Anga 601 KJ Meja Bryceson Msilu alieleza kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kushirikiana na TECO wamepanda jumla ya miti 3,400 kuanzia Disemba mosi mwaka huu na wanatarajia kupanda miti 3,000 ya matunda katika maeneo mbalimbali ya taasisi za umma jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...