Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo


NA K-VIS BLOG
WATEJA wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambao hawatumii mita za LUKU, sasa wanaweza kulipia bili zao za kila mwenzi kupitia benki ya NMB, na huduma hiyo inaanza kwa majaribio Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TANESCO Mikocheni jijini Dar es Salaam Desemba 15, 2017, Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo amesema, huduma hiyo ni kuwarahisishia wateja kuondokana na usumbufu wa kuzifikia ofisi za TANESCO kufanya malipo hayo na badala yake wanaweza kutumia benki ya NMB kufanya malipo.

“Tunaanza kwa majaribio katika kanda ya Dar es Salaam na Pwani na tukiona inakwenda vizuri tutapanua huduma hii kwenye mikoa mingine.” Alisema. Pichani Bw.Chowo (kulia), akitoa taarifa hiyo leo Desemba 15, 2017 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Tehama, Utafiti na utengenezaji mifumo, Evaristo Winyasi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...