Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika Wilaya za Kongwa na Kondoa mkoani Dodoma.

Katika ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika Jumatatu Desemba 11, 2017, Waziri Kalemani aliwasisitiza viongozi wa Halmashauri ambako Mradi wa REA III unapita, kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme hususan katika Taasisi mbalimbali za umma.

“Siyo vema Taasisi muhimu za umma zikaendelea kukosa umeme kwa kutokuwa na fedha hivyo kuwatesa wananchi. Hakikisheni mnatenga fedha kwa shughuli hiyo muhimu.”

Aidha, alibainisha kuwa, maeneo yanayopewa kipaumbele katika Mradi wa REA III ni Taasisi zote za umma ili kuhakikisha zinatoa huduma bora kwa wananchi.

Pia, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza Mradi huo katika maeneo mbalimbali nchini, kukutana na viongozi wa maeneo husika wakiwemo wabunge ili wapewe mwongozo wa sehemu muhimu za kipaumbele zinazotakiwa kuunganishiwa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeshika kipaza sauti) akiwasalimu wananchi wa Kijiji cha Pembamoto, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kifaa kinachotumika kuunganisha umeme katika nyumba pasipo kutandaza nyaya, kijulikanacho kama UMETA. Waziri alitoa kifaa hicho kama zawadi kwa baadhi ya wazee katika Kijiji cha Makole, Wilaya ya Kongwa, wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (kushoto), alipokuwa katika ziara ya kazi jimboni humo kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wataalam kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...