Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania BOT kuzifutia leseni benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi zitakazoshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha shughuli za kibenki nchini.

Ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania (COBAT).

“kwa taarifa niliyonayo hadi sasa baadhi ya benki hazijatimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha, hali ambayo haiwezi kuachwa iendelea hata kidogo, kwani haiimarishi sekta ya fedha na haiwasaidii wananchi kuendelea kiuchumi” alisema Waziri Kassim Majaliwa katika hotuba hiyo.Alisema Benki Kuu ilitoa muda hadi mwishoni mwa Desemba 2017, benki za wananchi ziweze kuongeza mtaji na kwamba muda huo hautaongezwa na wala Serikali haitatoa mtaji kwa benki hizo.

“Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania haitasita kuifungia benki yoyote na kufuta leseni yake ya biashara pindi itakapobaini inavunja sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi ambao unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja kama tulivyofanya kwa Mbinga Community Bank PLC kuanzia tarehe 12/5/2017” alisema Dkt. Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Maagizo hayo yamekuja siku moja baada ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango wakati akifungua tawi kuu la Benki ya CRDB mjini Dodoma, kuhakikisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, inazifuta benki zote zinazoshindwa kujiendesha kibiashara hata kama zinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihutubia katika mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika mjini Dodoma ili kujadili masuala ya Mitaji na Mpango wa Kuziunganisha Benki za Wananchi Tanzania.
Washiriki wa mkutano maalum wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mjini Dodoma.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Benard Kibesse (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi –COBAT, Bw. Rukwaro Senkoro, wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), mijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akifurahia jambo na Mbunge wa Mtwara Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia baada ya kufungua mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioshiriki mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi-COBAT, nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...