Na.WAMJW-Msalala

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto aweka historia kwa kutembelea Zahanati ya Mhandu kata ya Chela Wilayani Msalala ambapo tangu Uhuru wa Tanzania kijiji hicho hakijawahi kutembekewa na Kiongozi wa Kitaifa.

Waziri Ummy Mwalimu yupo ziara ya kikazi Wilayani Msalala kujionea Utekelezaji wa Mpango wa Malipo kwa Ufanisi(RBF) ambapo ulianza Januari 2016 kwa Mkoa wa Shinyanga

RBFni Mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi ambapo vituo vinapewa maeneo ya utekelezaji na kupimwa kuona kama wamekidhi na kufikiwa malengo hivyo kituo huhakikiwa na hatimaye kutolewa fedha kulingana na matokeo ya idadi za huduma zilizotolewa na ubora kulingana na miongozo ya utoaji wa huduma za Afya.Fedha zinazopatikana zinafanya maboresho ya vituo ikiwemo miundombinu ya kituo,madawa na vifaa tiba

Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika kutekeleza Mpango huo hata hivyo aliwataka watendaji kufanya uhakiki na kujiridhisha kwamba huduma za Afya zitolewazo zinakidhi viwango kulingana na miongozo ya Afya ndipo malipo yatolewe
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimsalimia mgonjwa aliyekuwa anasubiri huduma katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa dawa katika Zahanati ya Mhandu wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiangalia friji la kuhifadhia chanjo kwa ajili ya watoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelekezo juu ya upatikanaji wa dawa kutoka kwa mtoa huduma kushoto katika Zahanati ya Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na baadhi ya wazee wa kijiji cha Segese wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo ili kuangalia utekelezaji wa mpango wa malipo wa ufanisi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi.PICHA NA WIZARA YA AFYA –KAHAMA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...