Na Robert Hokororo, Kishapu DC

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imeendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo katika sekta ya elimu ya msingi kutokana na fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).

Itakumbukwa hivi karibuni ilitoa fedha kwa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ambapo pamoja na nguvu za wananchi imepiga hatua katika utekelezaji.

Baada ya kupokea kiasi cha sh. milioni 25 ujenzi wa nyumba ya walimu wawili pamoja na matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Idisanhambo ulianza mara moja na tayari umefikia hatua ya umaliziaji.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema pamoja na kupokea fedha kutoka TEA, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ya Kishapu imetenga jumla ya sh. milioni 90 kupitia mapato yake ya ndani kujenga nyumba sita za walimu.Magoiga alibainisha kuwa Halmashauri hiyo pia iliweza kupokea Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 88 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 11 za walimu.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Halmashauri imetenga jumla ya sh. milioni 48 kupitia mapato yake ya ndani kujenga matundu 24 ya vyoo kwa shule zake za msingi.Pia, Ruzuku ya Maendeleo (LGDG) sh. milioni 75 zitakazotumika katika ujenzi wa matundu 50 ya vyoo pia katika shule za msingi wilayani humo.

Fedha hizo kwa ujumla zinatarajiwa kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili katika sekta ya elimu ya msingi hususan upungufu wa nyumba za walimu na matundu ya vyoo.Aidha, pamoja na Halmashauri ikishirikiana na wadau kutekeleza miradi mbalimbali bado inaendelea kuhamasisha jamii kuchangia shughuli za maendeleo.

Pia kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya wazazi kuhusu masuala ya elimu, imeendelea kuelimisha jamii kuhusiana na suala hilo ili iendelee kupiga hatua wilayani humo.
Viongozi kutoka Idara ya Elimu ya Msingi wakiangalia maendeleo ya mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Idisanhambo ambao umefikia katika hatua za umaliziaji.
Afisa Elimu Ufundi katika Halmashauri ya Kishapu, Moshi Balele (kushoto) akitoa maelezo kwa viongozi wengine katika idara hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa choo katika shule ya msingi Idisanhambo.
Mojawapo ya vyoo katika shule hiyo ya msingi kikiwa katika hatua ya umaliziaji kabla ya kukabidhiwa na kuanza kutumika rasmi na wanafunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...