NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimesema mafanikio yliyofikiwa na Serikali ya awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ni kielelezo tosha cha kuenzi kwa vitendo Mapinduzi hayo ya Januari 12, mwaka 1964.

Udhibitisho huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ wakati akitoa tathimini yake juu ya hotuba ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein aliyoitoa katika kilele cha wamaadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi zilizofanyika Uwanja wa Amaan Mjini hapa.

Dk. Mabodi alisema mambo yaliyotajwa katika hotuba hiyo ni sehemu ya mafanikio ambayo kila mwananchi anatakiwa kujivunia kwani ni hatua ya maendeleo yanayotokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote.

Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza mambo mbali mbali ya kimaendeleo bila kujali changamoto na vikwazo vya kisiasa kwa lengo la kurahisisha upatanaji wa huduma za msingi kwa wananchi waliopo mijini na vijijini.

Alieleza kuwa mambo yaliyotolewa ufafanuzi wa kina ndani ya hotuba hiyo ya Dk.Shein ni pamoja na kuimarika kwa sekta ya uchumi ambapo makusanyo ya mapato yamefikia shilingi bilioni 548.571 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na shilingi bilioni 487.474 zilizokusanywa katika mwaka 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...