Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.

Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi, shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme.
Koka alitoa mchango huo, wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ,Miembesaba 'A'kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.Aliomba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi lengwa.

Akizungumzia changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni.

"Kulikuwa na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi""Lakini tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa awamu" alifafanua Koka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...