Na Mary Gwera, Mahakama

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya malipo yote ya huduma zake na ukusanyaji wa mapato kielektroniki ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na vilevile kuboresha huduma kwa manufaa ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso Januari 16, alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Mahakama kama ilivyo kwa Taasisi nyingine za Serikali imejiunga katika Mfumo huu ili kufanya ukusanyaji wa Mapato na malipo yote ya Huduma za Mahakama kufanywa kwa njia ya Kieletroniki, kwa hiyo ili kuwezesha matumizi ya mfumo huu yameandaliwa mafunzo haya maalum kwa Watumiaji katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi hii,” alifafanua Bw. Uisso.

Alitaja kuwa kwa kuanzia mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yameshirikisha jumla ya Watumishi 35 wa Mahakama kwa Mkoa wa Dar es Salaam, akitaja watumishi hao kuwa ni pamoja na Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Makarani kutoka Makao Makuu na ngazi zote za Mahakama kwa mkoa huu.

“Tunatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine kwa awamu, ili kuiwezesha Mahakama nchi nzima kutumia mfumo huu,” aliongeza Bw. Uisso.

 Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bi. Penina Henjewele akitoa Mada ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) kwa Washiriki wa Mafunzo hayo (hawapo pichani) 
 Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiongea jambo na Washiriki katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Sehemu ya Wahasibu na Makarani wa Mahakama wakiwa katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...