Na Jumbe Ismailly SINGIDA Jan,11,2018 Kuwekeza 


CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufuta ada katika shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini sekta ya elimu bado haijawekeza ipasavyo kwenye sekta hiyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kuikabili sekta hiyo mpaka sasa.

Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,Delphina Mngazija uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini.

Alifafanua kiongozi huyo wa kitaifa kwamba serikali inapowekeza kwenye sekta ya elimu kwa sasa ni lazima pia iwekeze kwenye matumizi ya kompyuta kwenye shule zilizopo na kuongeza kuwa elimu ya siku hizi inakwenda sambamba na mitandao ya kompyuta.

Kwa mujibu wa Prof.Lipumba nchi nyingi pamoja na nchi maskini zimewekeza mara tu watoto wanapoanza hujifunza pia kutumia kompyuta na kwamba matumizi ya kompyuta ni sawa kama vile kujifunza lugha.
“Mtoto mdogo ni mwepesi kujifunza lugha kuliko mtu mzima,hata mtu mzima ukiwa na simu mwanao anaweza kujua kuitumia ile simu kuliko wewe mtu mzima.

Na kuongeza pia kuwa wataalamu wa mambo ya watoto wanasema kuwa mtoto anapokuwa ndani ya tumbo la mama yake na kwa miaka miwili ya kwanza ndizo zinazompa mtoto fursa ya kujenga maungo yake,ya kujenga ubongo wake,ya kujenga kinga ya mwili.”alisisitiza Prof.Lipumba.
Prof.Lipumba hata hivyo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa vituo vya afya vilivyopo kuwa na virutubisho muhimu na kwamba kutokana na taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha.

“Kwa mujibu wa taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha,hawana madini ya chuma ndani ya damu yao hii inasababisha watoto wasipate lishe bora na watoto wa Tanzania wamedumaa.”alibainisha Mwenyekiti huyo.

Naye Katibu wa CUF Mkoa wa Singida,Selemani Ntandu aliwatahadharisha wanachama wa CUF pamoja na wale wa CCM waishio katika Kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla kwamba endapo watamchagua mgombea wa CCM,Justine Monko wakae wakijua kwamba makao makuu ya wilaya hiyo yatahamishwa kwenda Kijiji cha Sagarumba badala ya Ilongero.

Aidha katibu huyo alisisitiza kwamba wananchi wa jimbo la Singida kaskazini wanahitaji huduma bora za kijamii zinaboreshwa na kuonyesha masikitiko yake kwamba hivi sasa miundombinu ya barabara kwenye maeneo mengi hairidhishi kabisa jambo ambalo halishughulikiwi na watu waliokabidhiwa dhamana ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasilimia wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini alikwenda kumnadi mgombea ubunge wa chama hicha,Delphine Mngazija.
Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasisitiza wananchi wa vyama vyote vya siasa kumpigia kura mgombea wa chama hicho,Delphina Mngazija kwa kuwaonyesha mfano wa karatasi la kupigia kura
Mwenyekitti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Delphina Mngazija kwenye mkutano wa kampeni uliofanyia katika Kijiji cha Ughandi,Singida vijijini.
Mgombea ubunge wa CUF,Delphina Mngazija alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla na kuwaahidi kwamba endapo wataampaa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao atakwenda kupigania hadi kuondoa kero zinazowakabili wanawake wajawazito za kununua beseni,ndoo na mipira ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma vuilivyopo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ughandi wakimsikiliza mwenyekiti wa taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba alipokuwa nakiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ughandi kumuombea kura mgombea wa ubunge wa chama hicho ili aweze kuchagulia ifikapo jan,13,2018.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...