Na Grace Michael, Geita
MKUU wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa namna ulivyojipanga na unavyoshirikiana na Uongozi wa Mikoa mbalimbali kwa lengo la kuimarisha na kuboresha huduma za matibabu nchini.

Pongezi hizo amezitoa leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mfuko katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita.
“NHIF nawapongeza sana kwa namna ambavyo mmekuwa tayari wakati wote kuhakikisha huduma za matibabu zinakuwa bora zaidi na niwahakikishie tu kwamba Mkoa umejipanga kutoa huduma kwa wananchi ambazo ni za kiwango cha juu kwani kama viongozi tuna deni la kuwatumikia Watanzania,” anasema.

Injinia Gabriel aliutaka Mfuko kutochoka kutoa misaada kama hiyo ambayo inalenga kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Pombe John Magufuli imedhamiria kusogeza huduma kwa wananchi hivyo Mkoa unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za matibabu ili kuondokana na changamoto za huduma za afya.

Akikabidhi msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Anjela Mziray alisema jukumu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa Watanzania kupitia mfumo wa bima ya afya.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi. Anjela Mziray akionesha vifaa vya msaada vilivyotolewa na Mfuko huo katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akipokea vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 80 msada ambao umetolewa na NHIF.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akikalia kitanda kwa lengo la kukagua ubora wake.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akichunguza kitanda hicho na kuangalia ubora wa mashuka yaliyokabidhiwa.
 Baadhi ya Watumishi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...