Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

SERIKALI mkoani Pwani ,imemuagiza kamishna wa madini wa kanda ya mashariki ,kufuta leseni ya kitalu cha mawe ya kampuni ya Global Mining Company katika eneo la Kinzagu,Lugoba wilayani Bagamoyo kutokana na kushindwa kukiendeleza miaka 17 iliyopita.

Aidha ameagiza kufutwa kwa leseni iliyohodhi eneo la ofisi ya serikali ya kijiji cha Kinzagu na mhusika ananganywe mara moja.

Pamoja na hayo,ametoa wiki mbili kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,kumpelekea orodha ya leseni za vitalu vya mawe ambavyo vina mali za serikali .Mkuu wa mkoa wa Pwani,Evarist Ndikilo,alitoa maagizo hayo ,wakati alipokwenda kuingilia kati mgogoro baina ya mwekezaji Global co.ltd ,mwekezaji Gulf na wananchi katika kijiji cha Kinzagu. 

Alisema pia atawashughulikia wale wawekezaji wote ambao walikubaliana na serikali za vijiji lakini utekeleza baadhi ya mambo ambaoyo kwasasa wamekana makubaliano hayo.Ndikilo alisema ,kuanzia sasa eneo hilo liachiwe kampuni ya Gulf ambayo imeonyesha nia ya kuliendeleza eneo hilo na kulipa fidia wananchi 80 kwa fidia ya mil.540.2##

"Angalizo inawezekana Global Co.isiridhike hivyo ni haki yake kwenda kwenye vyombo vya sheria," Huku akae akijua mimi napeleka orodha ya wawekezaji wasioendeleza maeneo yao kipindi kirefu kwa waziri mwenye mamlaka husika.

"Tusibembelezane ,mkoa wa Pwani,sio shamba la bibi njooni mfanye maendeleo lakini msije na ghiliba ,mtu anachukua aneo anakaa nalo kama anatamia mayai????" alifafanua Ndikilo.Ndikilo alitaka orodha ya wawekezaji wanaohitaji kuendeleza maeneo ipelekwe ofisini kwake ili apeleke wizara ya madini na kupewa ridhaa ya kufanya maendeleo na sio ubabaishaji.

Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,alhaj Majid Mwanga alisema wameshughulikia mgogoro huo lakini kumekuwa na ugumu hali ambayo ilisababisha migogoro na kukandamiza maendeleo ya wananchi.Alizitaka serikali za vijiji kuandaa taarifa za wawekezaji waliokwapua ardhi za watu bila makubaliano na kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa vijiji.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,aliwataka wataalamu wa madini kusimamia haki za wananchi badala ya kunufaisha wawekezaji wasioitakia mema jamii.Alisema ,migogoro kati ya wawekezaji kwa wawekezaji inaumiza wananchi wasio husika.

Ridhiwani,aliipongeza serikali ya Mkoa huo kwa kufanya maamuzi hayo na kuchukua hatua yenye tija kwa wakazi wa Kinzagu.Kwa upande wake,Kamishna wa Madini wa Kanda ya Mashariki ,Julius Salota alisema atashughulikia maagizo hayo haraka iwezekanavyo.

Alisema watazungumza na kampuni ya Global ili kuangalia namna mbadala ya kumpatia eneo jingine .

Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,(pichani)alipokuwa akizungumzia mgogoro wa wawekezaji baina ya Global co.mining ltd na Gulf.Conc na wananchi wa kijiji cha Kinzagu kata ya Lugoba,Chalinze

Mwekezaji wa kampuni ya Gulf.Conc.Khaled Mohammed ,alipokuwa akizungumza mara baada ya mkutano wa kijiji Kinzagu kata ya Lugoba na mkuu wa mkoa wa Pwani,ambae ameingilia kati mgogoro huo ,na kutoa maelekezo na agizo kampuni ya Gulf. conc iendelee kuendeleza eneo lililokuwa na mgogoro na kulipa wananchi fidia ya mil.540 .2 ili kupisha eneo hill. (picha na Mwamvua Mwinyi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...