Na Mwamvua Mwinyi,Kisarawe

VYOMBO vya ulinzi na usalama,Mkoani Pwani vimetakiwa kuwatafuta baadhi ya watu wanaodhaniwa kuwa ni vigogo,; kuvamia msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe na kugawa viwanja.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ,alitoa rai hiyo wakati alipotembelea msitu huo kujionea baadhi ya maeneo ambayo yalivamiwa na wavamizi hao.Alisema vigogo hao wamesababisha msitu huo kuingiliwa na kuvamiwa mara nne na kundi la watu ambao wanadai sehemu ya msitu ni mali yao. 

Mhandisi Ndikilo ,alieleza kundi hilo limekuwa likiisumbua serikali kwa kwenda mahakamani na kushindwa .Aidha alisema vyombo hivyo vifanye ufuatiliaji kujua ni vigogo gani ambao wamekuwa wakiwatumia baadhi ya watu kwenda kushtaki mahakamani ili wapewe maeneo hayo kwa ajili ya viwanja .

“Inadaiwa kuna kampuni ilikata viwanja zaidi ya 300 na kuwauzia watu jambo ambalo haliwezekani kwani msitu huo umehifadhiwa kisheria”alisema mhandisi Ndikilo.Mhandisi Ndikilo,alisema kuwa msitu huo ulindwe kwani ni kama mapafu ya kupumulia viwanda na hewa ukaa hivyo endapo msitu huo utaharibiwa itahatarisha afya za watu. 

“Serikali ya mkoa haikibali hili,nimeshangazwa na kusikia kuna tume imekuja hapa Kisarawe na kuwahoji wataalamu mbalimbali juu ya suala la msitu huu wakati hakuna rufaa ya kesi ambayo ilifunguliwa na wavamizi ambao walishindwa”:;
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (Wa kwanza kushoto)na kaimu meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, Endrew Mwenuo (wa pili kulia)na mkuu wa wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ( Wa kwanza kulia) wakiangalia namna uvamizi ulivyofanywa na baadhi ya watu na vigogo katika msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe.
Kaimu meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)wilayani Kisarawe Mkoani Pwani, Endrew Mwenuo (kushoto) akimwelekeza jambo mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kuhusiana na uvamizi uliofanywa na baadhi ya watu na vigogo katika msitu wa Kazimzumbwi.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...