Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

Sekta Binafsi nchini imekiri kuwa uhusiano kati yake na Serikali umezidi kuimarika kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji na ufanyajibiashara hapa nchini kuliko ilivyokuwa hapo awali na kwamba hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kukuza ushiriki wa Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.

“Sekta binafsi imenituma kuleta pongezi kwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo utambuzi wa kwamba Sekta Binafsi ni mbia muhimu wa maendeleo ya Taifa letu” alisema Bw. Shamte.

Aliyataja baadhi ya mafanikio yanayo onekana bayana kuwa ni pamoja na kuinusuru Bandari ya Dar es Salaam kwa mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 hasa kuondoa VAT kwenye biashara ya mizigo ya kimataifa na kuondokana na umoja wa forodha ambao ulipunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bw. Shamte alisema kuwa majadiliano hayo kati ya Serikali na Sekta Binafsi kumeikoa sekta ya utalii hasa kwa kuondokana na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye leseni mbalimbali hatua ambayo imerejesha msisimko wa sekta hiyo.

“Serikali imepunguza pia mlolongo wa kodi kwa wakulima, japokuwa – kazi haijakamilika lakini mwanzo ni mzuri” aliongeza Bw. Shamte.Alieleza kuwa jitihada mpya na nzuri za kutatua changamoto za kodi kwa kampuni zinazojihusisha na biashara kati ya Tanzania Bara na Visiwani, na kuanza kufanya malipo kwa wakandarasi na watoa huduma wa ndani hatua ambayo wanaamini itakuza matumizi ya ndani na mzunguko wa fedha.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, akizungumza wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kuboresha masuala ya biashara na uwekezaji nchini, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifungua mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Serikali uliofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya Wawekezaji na wageni kutoka Taasisi za Kimataifa walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...