Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MMILIKI wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi na Mfanyabiashara, James Rugemarila wameomba madaktari wao kutoka India na Afrika kusini kuwepo wakati wakifanyiwa uchunguzi wa afya zao.

Maombi ya mshtakiwa, Harbinder Seth yamewasilishwa na Wakili wake, Alex Balomi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kupata taarifa kutoka upande wa mashtaka.

Akitoa taarifa hiyo mapema leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai kuwa alikwenda magereza kufuatilia hali za washitakiwa hao kama mahakama ilivyoagiza.

Swai amedai kuwa washitakiwa hao wameomba magereza wakati wanapofanyiwa uchunguzi kiafya madaktari wao kutoka nje ya nchi wawepo. 

Amesema, mshtakiwa Sethi ambaye anaishi na puto tumboni ambalo kwa uchunguzi aliofanyiwa na daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Desemba mwaka jana linatakiwa litolewe na, mshitakiwa alishirikishwa katika hatua hiyo lakini akaomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati wa kufanyiwa upasuaji.

Aisha amedai mshtakiwa huyo ameomba muda Wa kuwasiliana na daktari wake

Aidha amedai kuwa madaktari wa hapa nchini wamekubaliana na ombi la mshtakiwa ila wamesema kama afya ya mshitakiwa itaendelea kuathirika wataliondoa hilo puto.

Aliendelea kudai, kuhusu afya ya mshtakiwa Rugemalira, yeye anatibiwa na magereza pamoja na daktari wake anayeitwa Fred kutoka Hospitali ya Sanitas ambaye anachukua vipimo na kupeleka hospitalini kwake kisha kurudisha majibu magereza.

Alidai katika majibu hayo yanaonesha kuwa hana saratani kama alivyodai na kwamba serikali inafuatilia afya zao kwani hakuna jambo nyeti litakaloweza kuhatarisha maisha yao.
Wakili Balomi, akipinga hayo amedai, Hospitali ya Muhimbili wamethibitisha kuwa hawana uwezo wa kumfanyia upasuaji wa ama kuondoa au kuweka hilo puto na kusisitiza kwamba umuhimu wa daktari wake kutoka Afrika Kusini ni la kutiliwa mkazo kwani wamepokea maoni kutoka kwa madaktari hao Ka kusisitiza lazima wawepo wakati wa upasuaji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...