Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimewasili leo jijini Dar es Salaam kikitokea mkoani Kagera kilikokuwa na mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza na Michuzi Blog baada ya kuwasili leo,jijini Dar es Salaam katika uwanja kimataifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kocha Msaidizi wa Simba Massoud Djuma amesema kuwa anawashukuru wachezaji wake kwa kufanya vizuri kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Amesema anaamini watafika mbali wakiendelea kucheza kwa kumsikiliza Mwalimu. Aidha Mwalimu huyo amewapongeza wachezaji kwa jinsi wanavyojituma." Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu tumerejea salama, pia niwapongeze wachezaji wangu kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu, naimani tukicheza kwa ushirikiano tutazidi kufanya vizuri zaidi na zaidi,"amesema Masoud 

Wakati huohuo mchezaji Shomari Kapombe baada ya takribani miezi sita aliyokuwa akiumwa jana amepata nafasi ya kucheza na ameonesha kiwango kikubwa katika mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar na kutengeneza nafasi ya goli la pili ililofungwa na John Bocco dakika ya 79.

Kapombe amesema kuwa anamshuru mwalimu (Massoud Djuma) kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza mchezo wa jana na anaamini ataendelea kufanya vizuri katika Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.


 Mchezaji wa wekundu wa Msimbazi SimbaSc Shomari Kapombe akizungumza na waandishi wa habari alipowasili leo Jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere.
Kocha Msaidizi  wa Simba Massoud Djuma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwa sili leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa kimataifa Mwalimu J.K. Nyerere akiwapongeza wachezaji ea Kikosi hicho kwa kufata maelekezo yake  na kufanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...