Muonekano wa leo wa tuta la kutandazia reli ya kisasa (Standard Gauge) katika eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam ulivyo sasa, ikiwa ni hatua iliyofikiwa katika muendelezo wa ujenzi wa reli hiyo ulioanza  mwezi Desemba mwaka jana katika mradi unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu na utajengwa kwa awamu nne. Reli inatarajiwa kutandikwa baada ya tuta kukamilika.
Kampuni Hodhi ya rasilimali za reli nchini (RAHCO) ndiyo inatekeleza mradi huo kutoka Dar es salaam kwenda Isaka na Mwanza imegawanyika katika awamu ndogo nne ikiwemo Dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutupora hadi Tabora na Tabora hadi Mwanza. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Injinia Masanja Kadogosa jumla ya makandarasi  wanne wanaendelea na kazi usiku na mchana ili kukamilisha  ujenzi wa reli hiyo yenye upana wa mita 1.345 na ambao utaruhusu treni kutembea kwa spidi ya kilomita 160 kwa saa. 
Mradi huu mkubwa unatarajiwa  kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususan maeneo ambapo reli hiyo itapita ikiwemo  nchi  jirani ya Rwanda ambayo imekubali kujenga aina hiyo ya reli toka Isaka hadi Kigali. Mtandao mzima wa reli nchini unaotegemewa kujengwa kwa kiwango cha standard Gauge una jumla ya kilometa 2,561 ukitarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 7.6i Bilioni 7.683.  
 Eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam. Ujenzi huu ulianza rasmi mwezi Desemba mwaka jana ambapo kazi iliyopo ni kusafisha njia na kujenga hilo tuta  kabla ya kuanza kutandaza reli.
 Tuta linavyoonekana katika eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
 Sehemu ya tuta la kupitishia reli eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam
 Sehemu ya tuta la kupitishia reli eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...