Wakala unapenda kuujulisha umma kuwa Serikali ya Tanzania haijapiga marufuku biashara na matumizi ya mkaa, isipokuwa inachotaka ni kuona uvunaji misitu unafanywa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizotungwa. Serikali inataka watu wafanye biashara hiyo kwa njia halali na walipe ushuru na kodi kwa mujibu wa sheria.

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wanatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:
(i) Awe na hati ya usajili;
(ii) Awe na hati ya usafirishaji wa mazao ya misitu (Transit Pass);
(iii) Awe na leseni ya kuvuna mazao ya misitu;
(iv) Awe na leseni ya biashara ikiwa ni pamoja na TIN namba;
(v) Alipie ushuru wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kama ilivyobainishwa kisheria;
(vi) Awe na daftari la kumbukumbu ya kupokea na kuuza mazao ya misitu.
Kutokana na Kanuni za usafirishaji wa mazao ya misitu za mwaka 1999 hairuhusiwi mtu yeyote kusafirisha mazao ya misitu (kwa njia ya barabara au maji) kati ya saa kumi na mbili jioni na saa kumi na mbili asubuhi.
Atakayevunja masharti hayo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkaa.
Hairuhusiwi mtu yeyote kusafirisha mkaa hadi atimize masharti yaliyoko hapo juuu. Vilevile, mkaa, hata kama ni mfuko mmoja kwa ajili ya biashara au matumizi ya nyumbani, sharti ulipiwe.Pamoja na kutimiza masharti yaliyoorodheshwa hapo juu, wafanyabiashara wa mkaa wanatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-


(i) Awe na leseni itakayotolewa na Afisa Misitu wa Wilaya au Wakala wa Huduma za Misitu;
(ii) Awe na hati ya kusafirisha mkaa (Transit Pass), ambayo itagongwa muhuri katika kila kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu.
(iii) Mkaa usafirishwe kupitia njia zilizoruhusiwa na Ofisi za Misitu.
(iv) Atatakiwa alipie ushuru wa Serikali kwa kila kilogramu moja Sh 250 au kilogramu 50 kwa Sh 12500.
Kwa mtu yeyote atakayesafirisha mkaa bila kutimiza masharti yaliyotajwa hapo juu, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Maelezo zaidi yanapatikana katika ofisi za Misitu za Wilaya na TFS.

Haya sio matenga ya samaki la hasa ni mbinu mpya iliyobuniwa na wahalifu  wanaosafirisha mkaa kinyume na taratibu kama yalivyokutwa na maafisa Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kanda ya Mashariki walipokuwa wakifanya doria eneo la Dumila barabara ya Domoma - Morogoro jana.
 
kulia ni Herman Awet Afisa Misitu kanda ya mashariki akiwa na  henry malya ambaye anasimamia safu ya Dumila wakimueleza Mama mfanya biashara (aligoma kutaja jina lake) taratibu za bishara na usafirishaji wa mkaa mara baada ya kumkamata kwa kosa la kukiuka taratibu za usafirishaji mkaa kwa kuweka mkaa huo kwenye matenga na kusafirisha kama matenga ya samaki ili kukwepa maduhuli ya Serikali. Mama huyo alikamatwa Barabara ya Dumila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...