Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokea jumla ya Wanachma wapya 350 katika Kongamano Maalum lililoandaliwa na Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Kheri amewataka Vijana wanaopata nafasi za uongozi kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuwakomboa wengine na kuacha kutumika na makundi ya watu.

“Vijana wengi ambao wameaminiwa wameacha kushughulika na matatizo ya Vijana na yenye tija kwa taifa, wamekuwa wakiendeshwa na watu ambao wanamaslahi yao binafsi” amesema Kheri

Amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeweza kuwaamini Vijana, hivyo kila kijana wa CCM  anabudi kuwaunga mkono viongozi wote Vijana ambao wana nia ya dhati ya kutaka kulifikisha taifa hili pale linapotakiwa liwe.

Alimaliza kwa kutoa wito kwa Vijana wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Chaguzi ndogo zinazoendelea na kuifanya CCM ishinde kwa kishindo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Chama Cha Mapinduzi(UVCCM),Kheri James akizungumza na Wanachama wa Umoja huo Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika ukumbi wa Urafiki leo jijini Dar Es Salaam .
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka, akisalimiana na Mmoja ya Wanachama wapya waliojiunga na Chama hicho kupitia Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sehemu ya wanachama wapya 350 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi Tawi la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Wakila Kiapo cha Uaminifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...