Wananchi wa Mbamba Bay wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay (km 67), kwa kiwango cha lami ili kutatua changamoto za usafirishaji wa abiria na mizigo wanazozipata hususan katika kipindi cha masika.

Wananchi hao wametoa kero hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, alipofika wilayani hapo kukagua barabara hiyo ambapo wamefafanua kuwa licha ya wilaya hiyo kuwa na maliasili nyingi, wawekezaji na wafanyabiashara hushindwa kufika kutokana na changamoto ya barabara, hivyo kupelekea uchelewaji wa maendeleo katika wilaya yao.

"Uduni wa barabara hii unapelekea kutopata maendeleo ya haraka, pia usafiri kutoka hapa kwenda maeneo mengine ya jirani huwa mgumu hususan katika kipindi cha mvua kwani madereva wengi hupandisha nauli", amesema mmoja wa wakazi wa Mbamba Bay, Bw. Bahati Ndege.

Aidha, wananchi hao wameipongeza Serikali kwa hatua zinazofanya katika utatuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo wamefafanua kuwa Serikali kuamua kujenga barabara ya lami kutaboresha uchumi katika wilaya yao na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (mbele), akishuka ngazi wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa unaojengwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma na kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Edwin Nunduma, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu hatua na changamoto wanazozipata katika miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukagua miradi ya ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba ya makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma. Miradi hiyo inajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Muonekano wa hatua ya awali ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Mradi huo unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Ruvuma, Eng. Lazeck Alinanuswe (kulia), wakati akikagua barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa KM 67 inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO. Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa tarehe 11 mwezi Disemba mwaka jana.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...