Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

WATU saba akiwemo aliyekuwa fundi wa bomba la mafuta la Tazama, Samwel Nyakirang'ani (63) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia bomba la mafuta.

Nyakirang'ani anashtakiwa pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ufukoni, Nyangi Matoro (54), washtakiwa wengine,
Mfanyabiashara Farijia Ahmed (39), Malaki Mathias (39), Kristomsi Angelusi(25), Henry Fredrick (38) na fundi ujenzi Pamfili Nkoronko(40).
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Tulumanywa Majigo akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu Peter Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba.Wanadaiwa kutenda makosa yanayowakabili chini ya sheria petrol kinachoenda pamoja na sheria ya uhujumu uchumi.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili Majigo alidai kuwa kosa la kwanza ni kujiunganishia isivyo halali katika bomba la mafuta ya Dizeli.

Imedaiwa, washtakiwa wote  katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 na Januari 8, mwaka huu, huko maeneo ya Tungi Muungano katika Wilaya ya  Kigamboni jijini Dar es Salaam walijiunganishia bomba la upana wa inchi moja kwenye bomba la inchi 24 la  diesel material yasiyoshika kutu bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Katika shtaka jingine la kuharibu miundombinu ( kifaa kinachotumika kwa ajili ya utoaji huduma muhimu)  imedaiwa katika tarehe na maeneo hayo hayo, washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la Inchi 24 linalotumika kusambaza mafuta ya Dizeli mali ya TPA.

Washtakiwa hao wanadaiwa pia kuwa, kati ya 2015 na January 8, 2018 maeneo ya Tungi Kigamboni, walitoboa bomba la inchi 28 la mafuta linalotumika kwa ajili ya usambazaji wa  Crude Oil likiwa ni mali ya TPA.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Majigo alidai Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao.
Washtakiwa hawaruhusiwi kujibu lolote kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu Uchumi ma imeahirishwa hadi Januari 30,2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamili, washtakiwa wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...