Na Jumbe Ismailly -SINGIDA.

NAIBU Waziri wa maji,Juma Aweso amewaagiza wataalamu wa maji nchini kuwasimia kwa karibu wakandarasi waliopewa kazi za miradi ya maji katika suala zima la utekelezaji wa miradi hiyo na kuwaahidi kwamba wizara hiyo haitaweza kuwa kikwazo katika kuhakikisha wakandarsi hao wanalipwa fedha zao kwa wakati ili miradi hiyo isikwame.

Naibu Waziri huyo alitoa agizo hilo mjini Singida wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Singida kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Aidha Aweso alisisitiza kwamba katika ziara zake anazoendelea kufanya amebaini kwamba matatizo ya upatikanajai wa huduma ya maji safi na salama haiwezi kupatikana kwa wataalamu wa wizara hiyo kukaa ofisini kwa kuchezea kompyuta,bali maji yanapatikana kwa wananchi kutokana na kuwatembelea wananchi na kubaini kero zao.

“Na tunafanya ziara tukitambua kabisa maji hayapatikani kwa kukaa ofisini kwa kuccheze kompyuta,maji yanapatikana kwa wananchi kwa sababu anayelala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo ya mgonjwa.”alifafanua Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo Aweso aliweka bayana kwamba akiwakatika ziara yake ya wiki moja Mkoani Shinyanga alibaini baadhi ya miradid iliyokuwa ikisuasua lakini baada ya kuisukuma imeanza kwenda vizuri na hivyo kutumia fursa hiyo kuwaahidi wananchi wa Mkoa wa Singida kwamba anatarajia kurudi Mkoani hapa kufanya ziara katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.
Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso akiteta jambo na katibu wake mara baada ya kupokea taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Singida inayohusu sekta ya maji.
kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Faustine Kiyui akisoma taarifa ya sekta ya maji ya Manispaa ya Singida kwa Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso.
Naibu wazziri wa maji,Bwana Juma Awesso akiongozaa kikao cha watendaji wa Halmashauri ya wilaya na Manispaa ya Singida baada ya kupokea taarifa za Halmashauri hizo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Ni baadhi ya watendaji wa serikali wa wilaya ya Singida wakiwa katika kikao cha pamoja na Naibu waziri wa maji,Bwana Juma Aweso kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...