WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.

Aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.

“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...