WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wizara yake haina mpango wa kuongeza tena muda zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwataka wafugaji popote walipo nchini kupaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa ng’ombe na punda wote wamepigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.

Pia Waziri Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikali kuwakatalia wafugaji kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa sio wakazi halali wa maeneo husika jambo ambalo amesema halikubaliki na kusisitiza kuwa zoezi lisihusishwe na migogoro ya muda mrefu ya matumizi ya ardhi na hivyo kuagiza kuwa ng’ombe na punda wote nchini wapigwe chapa isipokuwa ya kutoka nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi upigaji chapa mifugo, Mpina alisema hadi kufikia Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo wameshapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali.

Aidha amesema wafugaji wote nchini wataoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26 huku akizionya halmashauri ambazo zitashindwa kutekeleza kikamilifu hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi wake.

Alisema hadi sasa halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 huku halmashauri 9 zikiwa bado hazijaanza kabisa zoezi hilo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo mjini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Waziri wake Mhe.Abdalah Ulega na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili yakutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Joelson Mpina akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara hiyo Mjini Dodoma leo. Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kutoa tathimini ya zoezi la upigaji chapa mifugo baada ya kumalizika kwa siku 15 za awali baada ya muda wa nyongeza wa siku 30 uliotolewa na Waziri Mpina. Kulia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, Mashimba Ndaki. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...