KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakuwa mgumu na watacheza kwa umakini ili waibuke na ushindi.

Azam FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakitoka kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumapili.

Cioaba amesema Yanga ni moja ya timu kubwa nchini ikitoka kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita na kudai kuwa wataingia uwanjani na kuonyesha uwezo mkubwa.

“Mechi itakuwa Chamazi, hautakuwa mchezo mwepesi nitakuwa na muda wa siku tatu wa maandalizi kwa kuwa nina safari ndefu sana na wachezaji wanauchovu kidogo lakini siku hizo tatu nitawaunganisha vema wachezaji na kujaribukufanya vizuri dhidi ya Yanga Chamazi, sihitaji kupoteza mchezo wowote hapo baadaye,”amesema.

Hadi sasa ikiwa imecheza mechi 14 za ligi, Azam FC imefanikiwa kuwa rekodi bora baada ya kutopoteza mchezo hata mmoja, ikiwa imeshinda mechi nane na sare sita ikiwa kileleni kwa pointi zake 30 ikiizidi mechi moja Simba ambayo ipo nafasi ya pili ikijikusanyia 29.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...