Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kamati Tendaji ya chama cha soka Wilaya ya Magharibi A Unguja inatarajia kukutana kwa siku 2 na makundi mbalimbali ya wadau wa soka wilayani humo ili kujadili mambo yanahusiana na msimu wa ligi wa 2017/18.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ZFA hiyo Zainab Omar Mussa, Kamati itakutana na waamuzi waliochezesha ligi hiyo kabla ya kwenda katika mapumziko na wajumbe wa Kamati ya waamuzi kitakachofanyika Jumamosi ya Januari 20, 2018 kitakachofuatiwa na mkutano wa vilabu vyote wilayani hump kitakachofanyika Jumapili Januari 21, 2018.

Alisema vikao hivyo ni utekelezaji wa uamuzi wa vikao vya Kamati Tendaji na Sekretarieti ya ZFA hiyo ambavyo vilielekeza kufanyika vikao hivyo ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kipindi kilichopita.

Akizungumzia mwendelezo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 31 katika daraja la pili na 12 za daraja la tatu, Zainab alisema ligi hiyo itaendelea kuanzia Januari 27, 2018 na ratiba kwa ajili ya ligi hiyo itatolewa siku ya kikao na vilabu na kuvitaka vilabu vyote kuhudhuria sambamba na kuanza maandalizi ya Timu zao kwa ajili ya ligi hiyo.

Msimu wa ligi katika wilaya ya Magharibi A ulianza rasmi mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2017 na kusimama mnamo mwezi wa 12 ili kupisha mashindano ya kombe la Mapinduzi na dirisha dogo la usajili lililomalizika hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...