Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakiangalia bidhaa mbalimbali za uchongaji na ushonaji toka kwa wajasiriamali wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha shirikisho hilo  jana katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (katikati) akiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika Ahmad Ahmad na kulia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Wallace Karia.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akivalishwa urembo wa mkononi wenye rangi za bendera ya Taifa mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino (aliyevaa shuka la kimasai) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Leodger Tenga mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) tayari kwa kikao cha shirikisho hilo mapema  jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mkuu toka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza (kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino, zawadi mbalimbali toka bodi hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirikisho hilo mapema jana katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.Picha na Idara ya Habari – MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...