Uongozi wa Halmashauri ya Wilayaya Handeni umekabidhiwa rasmi mradi wa choo cha matundu sita kilichojengwa na shirika lisilo la Kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) lenye thamani ya Milioni 19 za Kitanzania  kwa lengo la kuboresha huduma ya vyoo kwa wanafunzi wa shule za Msingi. 
 Akipokea mradi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Aweso Bakari ( Afisa Tarafa Mkumburu) alisema kuwa anashukuru sana CDMT kwa kuona uhitaji wa Shule ya Masatu na kuamua kusaidia ujenzi wa choo chenye  matundu 6 yatakayosaidia kupunguza changamoto ya vyoo shuleni hapo.

Kaimu Mkurugenzi alisema kuwa, Shule ya Masatu kwa mujibu wa ripoti ya Mwalimu Mkuu ilikuwa na upungufu wa matundu 29 ya vyoo, Hivyo kwa mradi wa matundu 6 yaliyojengwa na Shirika la CDMT umepunguza na kufikia matundu 23, hivyo  anashukuru Shirika hilo  kwa jitihada za kuunga Mkono Serikali katika ujenzi wa miundombinu.
 Aidha aliwataka viongozi wa shule na Kijiji kuhakikisha wanatunza mradi huo kwa kuzingatia usafi wa mazingira ili hata waliofadhili mradi huo wakija kuutazama wafarijike na waweze kuisaidia Serikali kutatua changamoto nyingine ambazo bado zinaikabili shule hiyo.

“Naishukuru sana CDMT, Viongozi wa shule na Kijiji msimamie mradi huu vizuri kuhakikisha hauharibiwi kwa michoro ya ajabu na usafi uzingatiwe ili hata wafadhili wakija kutembelea waone thamani yake” alisema Aweso
 Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Segera Mh. Yassin Mtamike alisema kuwa, anaishukuru CDMT na yeye kama Diwani atahakikisha mradi huo unatunzwa na kulindwa ili kuwapa nafasi wafadhili waweze kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu.
 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) na Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Emile Philipo alisema kuwa baada ya kufika Handeni aligundua changamoto ya vyoo bora kwa Shule za Msingi na kuamua kuandika andiko la kuomba msaada kwa Serikali ya Marekani yenye fungu la fedha la Rais wa Marekani linalosaidia Afrika kwa lengo la kupunguza changamoto ya vyoo.
 Aliongeza kuwa kwa tafiti zake  za awali aliamua kusaidia shule tatu za msingi ambapo shule  mbili za Msomera na Masatu zipo Hamashauri ya Wilaya ya Handeni na shule moja  1 ya Seuta Halmashauri ya Mji Handeni.

Miradi yote imekamilika kwa jumla ya Milioni 58 za Kitanzania ambapo kila shule imejengewa matundu 6 ikiwa matundu 3 kwa  wanafunzi wa kike na 3 kwa wanafunzi wa kiume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...