Na Emmanuel ,Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Felix Lyaniva amewataka madereva wa pikipiki na Bajaj kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto.

Amesema lengo ni kuepuka ajali zinazosababishwa na madereva wazembe na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Lyaniva ameyasema hayo jana , wakati wa utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaji katika vituo vyao mbalimbali katika katika Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu uliofadhiliwa na Diwani wa Kata hiyo Abdallah. 

Diwani huyo ameshirikiana na Kampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaji Association (TAMOBA) kwa ajili ya kuzisajili Pikipiki na Bajaji katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi.Akizungumza zaidi Lyaniva amewapiga marufuku mgambo wa wilaya hiyo kutokamata pikipiki na Bajaj kwani wengi wao wamekuwa wakikamata pikipiki hizo bila ya kuzingatia sheria.

Amesena kazi ya kukamata bodaboda itafanywa na askari wenye weledi na wenye kujua sheria za usalama barabarani.Lyaniva pia amewapongeza TAMOBA kwa kuwafikia madereva bodaboda na bajaj kwani walikuwa na wasiwasi wa kuibiwa vyombo vyao na kuporwa na majambazi.

Ameongeza Diwani huyo ameleta maendeleo makubwa na mazuri katika Kata hiyo na pia TAMOBA imeleta usalama mzuri kabisa wa kisasa kwa kuwa madereva hao watafanya kazi zao wakiwa hawana wasiwasi wa kuibiwa Pikipiki zao na mali zao wawapo katika majukumu yao hayo pamoja na abiria wao.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaniva akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kuzingatia sheria za usalama Barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu na viatu wakati wanapoendesha vyombo vya moto,jana jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza na akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo, jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Utumishi wa TAMOBA Bw. Erasto Lahi akizungumza na madereva wa pikipiki na Bajaj juu ya kuzisajili Pikipiki na Bajaj katika mfumo wa GPS utakaowawezesha kujua Pikipiki iliyoibiwa ipo eneo gani na kuweza kupatikana kwa haraka zaidi, jana jijini Dar es Salaam.
Semu ya madereva wa pikipiki na Bajaj piki na Bajaj wakiwa kwenye mkutano utambulishaji rasmi wa mfumo wa namba utakaowatambulisha madereva pikipiki na bajaji katika vituo vyao mbalimbali vya Kata ya Kibondemaji, Mbagala Jijini Dar es salaamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...