Na Fredy Mgunda,Ileje 

HALMASHAURI ya wilaya ya Ileje mkoani songwe imetumia zaidi ya shilingi milioni mia moja themanini katika ujenzi wa madarasa kwa kutumia fedha za EPFR ambazo hutolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukagua miradi hiyo,mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi alisema kuwa jukumu la uongozi ni kuhakikisha kuwa pesa inayotolewa na serikali inatumika kama ilivyokusudiwa na serikali kuu kwa faida ya sekta ya elimu.

“Serikali inatoa pesa nyingi sana hivyo tusipo simamia vizuri pesa hizi zitapotea kitu ambacho Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Maguli hataki kabisa kusikia kuna pesa ambayo haitumiki kama ilivyokusudiwa ndio maana nimeamua kuanza kukagua miradi yote ambayo inatekelezwa katika halmashauri yetu” alisema Mnasi 

Mnasi aliwaomba wananchi kuchangia nguvu zao kuhakikisha shughuli za ujenzi wa madarasa na vituo vya afya wanajitolea vilivyo ili kuendelea kufanya kazi sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano.“Mimi binafsi nawaomba wananchi wajitolee kufyatua tofali ,kuchota maji,kubeba mchanga na kusomba tofali ambazo zinakuwa zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya ujenzi ambao utakuwa na faida kwao na vizazi vijavyo” alisema Mnasi
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu na kuhakikisha wananchi wanachangia nguvu zao kuleta maendeleo kwenye vijiji vyao
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitendo alivyokuwa anafanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu 
 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Ileje Haji Mnasi akibadilisha mawazo na baadhi ya viongozi walikuwa kwenye eneo la ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Izuba na shule ya msingi Ilulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...