Na Hamza Temba - WMU-Bagamoyo, Pwani
....................................................................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha
hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili
iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.
Ametoa
agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani
yake pia kuna mapito ya wanyamapori.
Dk.
Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa
jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha
na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi
hiyo kwa asilimia 100.
"Sisi
kama jamii tumeshindwa, tunaomba msaada wa Serikali, itusaidie kuondoa hawa
wavamizi na ikiwezekana ichukue jukumu la kulinda hifadhi hii kwa asilimia
100," alisema Tofiki.
Alisema
jumuiya hiyo ambayo ni muunganiko wa vijiji 24 inakabiliwa na changomoto kubwa
ya ujangili uliokithiri ambao umepelekea kuuwawa kwa wanyamapori zaidi ya
asilimia 90 ya waliokuwepo tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 1997.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...