Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
..........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria

"Nimeagiza watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.

"Kwasababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama"  alisema Dk. Kigwangalla.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu Waziri Kigwangala wa ajabu kabisa,anadiriki kuwaambia hawa wafugaji waandae maonyesho ya kimataifa wakati wizara yako imewafungia biashara yao ya kuuza nje haoni hata haya.wafugaji hawa wapo katika uchungu wa kufungiwa biashara yao ya vipepeo wanaozalisha ambao maisha yao ni siku saba tu,kwa kweli serikali za kiafrika huwa zinadhulumu na kuwaingiza katika umasikini watu wao.ni haki yao kutafuta njia mbadala kama hiyo ya kutafuta dhahabu katika msitu huo wa Amani kwa maana juhudi zao za kuondokana na umasikini zinakwamishwa na serikali hii yenyewe.walikuwa wanaingiza dola 90000 kwa mwaka sasa hawazipati.wafanye nini???

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Adadi mbunge wetu wa Muheza mweleze huyu waziri Kigwangala wananchi wa Amani tumechoka na siasa za kuchangia kutuingiza kwenye umasikini.wakati serikali haijaingiza (investment) yoyote katika uzalishaji wa vipepeo hawa uzalishaji unaofanywa na wananchi masikini tena wa chini kabisa ,leo wanafungiwa kutouza nje bila sababu zozote za msingi.huu ni uonevu unaofanywa na serikali hii ya awamu ya tano kwa masikini hawa wanaotafuta riziki kwa juhudi zao na leo unawafungia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...