Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam imesema imetumia zaidi ya Sh.bilioni 5.5 kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo  kwa bajeti ya kuanzia Julai mwaka 2017 hadi Desemba mwaka huo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu amesema fedha hizo zimetumika katika utekelezaji wa miradi inayohusisha  ujenzi wa vyumba  vya madarasa ,vyoo na hosteli.

"Kwa upande ya elimu ya msingi  shule mpya  nne zimejengwa kutokana na ongezeko la wanafunzi na ongezeko la wanafunzi ambalo limetokana na mpango wa Serikali wa elimu bila malipo,"amesema.

Pia  ametaja kuwa katia mpango huo madarasa 28 yamejengwa katika shule za msingi Bonyokwa, Mongo la ndege, Mbondole, Mji Mpya, Kibaga, Bangulo na Misitu. "Madarasa sita yamefanyiwa ukarabati darasa moja Kinyerezi na Mchikichini vyumba vitano" amesema Tabu.

Amesema katika fedha hizo jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule hizo huku matundu 40 yakiwa katika shule za zamani na yaliyobakia katika shule mpya.

Shaibu ameongeza pia fedha hizo zimetumika kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali ili kukabiliana na changamoto ya usafiri wa wanafunzi wanaokaa maeneo ya mbali na shule.

Aamesema halmashauri imefanya ukarabati wa huduma za mama na mtoto katika zahanati ya Msongola na Mvuti kwa kutumia mapato ya ndani ikiwa pamoja na ukamilishaji na ukarabati wa miradi ya maji katika kata ya Minazi, Tabata, Majohe, Vingunguti, sekondari Pugu, Mkera na Pugu stesheni.

Amesema katika kipindi hicho halmashauri imepeleka kiasi cha Sh. 543,400,000 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu na kukarabati miundombinu ya jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP.
 Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza juu ya taarifa ya utekelezwaji wa bajeti ya Halmashauri hiyo katika kipindi cha julai hadi Desemba 2017.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini Taarifa hiyo ambayo inatolewa na Tabu Shaibu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...