Na Stella Kalinga, Simiyu
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA),  Richard Mayongela ameiomba serikali kutoa kiupaumbele cha ujenzi wa Viwanja vya Ndege kwa mikoa ya Simiyu na Lindi katika bajeti ya mwaka 2018/2019 ili kuongeza fursa za uwekezaji na utalii. 
Mayongela ametoa ombi hilo katika kijiji cha IGEGU kata ya Sapiwi wilayani  BARIADI katika eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Prof. Makame Mbarawa mkoani Simiyu. 
Amesema hatua za awali za maandalizi ya ujenzi wa Uwanja huo zimekamilika ambapo usanifu na upembuzi yakinifu vimeshafanyika na makadirio ya awali yanaonesha kuwa mradi huo utagharimu takribani shilingi bilioni 95.56 na utakapokamilika utawezesha ndege zenye uwezo wa kubeba  kuanzia watu 75 na kuendelea kutua.
Ameongeza kuwa Ujenzi wa Uwanja huo utakapokamilika utakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Mkoa huo katika nyanja za uchumi na utalii  na utachangia kuufungua mkoa wa Simiyu kiuchumi pamoja na mikoa mingine ya kanda ya Ziwa. 
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kukamilika kwa Uwanja huo itakuwa ni faida kubwa kwa kuwa utakuwa  Uwanja pekee wa Serikali hapa nchini ambao Watalii watautumia kuifikia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa urahisi kuliko viwanja vingine.  
“Tunajenga Uwanja ambao kimkakati unakaa mpakani mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, karibu na uwanja huu kuna hii barabara ya inayotunganisha na Mkoa wa Shinyanga kupitia Malampaka ambako kutajengwa Reli ya Kisasa, hapa jirani  tuna eneo ambalo tutajenga Kiwanda cha Vifaa tiba, mbele yeke tunaanzisha Kanda ya Nanenane ...tunaamini kukamilika kwa mradi huu kutakuwa na faida sana  kwa Serikali na wananchi”  alisema Mtaka.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini,  Richard Mayongele (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(mwenye kofia)  kuhusu Uwanja wa Ndege wa mkoa wa Simiyu unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Waziri huyo leo Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akieleza juu ya umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa mkoa unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa  akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Simiyu, unaotarajiwa kujengwa Kijiji cha Igegu wilayani Bariadi wakati wa ziara yake leo Mkoani humo.
 Mkuruugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela akiwasilisha taarifa ya eneo la Igegu wilayani Bariadi linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege Mkoani Simiyu  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa alipokuwa kwenye ziara mkoani humo leo.
Diwani wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi akimweleza jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe. Prof. Makame Mbarawa(kushoto) alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Ndege Mkoani Simiyu, wakati alipokuwa katika ziara Mkoani Simiyu leo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...