Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia  Juma Nyoso wa Kagera Sugar kwa kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

Akitolea ufafanuzi hukumu hiyo, Ofisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kamati ya nidhamu iliketi na kujadili masuala mbalimbali ya nidhamu ikiwemo suala la beki wa timu ya Kagera Juma Nyoso kumpiga shabiki wakati wa mchezo wao dhidi ya Simba uliochezwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Ndimbo amesema  "Kamati ya nidhamu ya TFF iliweza kukaa na kulijadili masuala mbalimbali ya nidhamu pia  ilijadili shauri ambalo lilifikishwa kwenye kamati hiyo ambalo lilimuhusu mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyoso kuhusu tukio lake ambalo lilitokea kwenye mchezo uliozikutanisha Kagera Sugar na Simba kwenye uwanja wa Kaitaba," amesema.

Katika kesi hiyo Nyoso alituhumiwa kwa kosa la kumpiga shabiki na kupelekea kupoteza fahamu baada ya kumalizika kwa mchezo kinyume na kanuni za ligi kuu zinazozungumzia uungwana katika mchezo wa kosa 'Fair Play'.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Kamati waliweza kupitia ripoti ya kamishna wa mchezo huo ambapo imeweza kuelezea  tukio hilo ambapo  Nyoso wakati anaelekea vyumbani aliweza kupishana na shabiki aliyekuwa anapuliza vuvuzela na kusababisha Nyoso kusimama na kuanza kumpiga shabiki huyo kwa kutumia kiatu na baadaye akamuinamisha na kuanza kumpiga kwa kutumia goti.

"Kwa upande wa Kamati iliweza kumuita Nyoso na kujitetea na kwa upande wake alikana madai yanayomkabili ya kumpiga shabiki na kudai kuwa amlikunja na sio kumpiga," amesema Ndimbo

Baada ya kumsikiliza utetezi wake Kamati imeweza kumtia hatiani Nyoso kwa kupitia kanuni ya ligi kuu na pia waliweza kupitia  taarifa za nyuma za mchezaji huyo na kuona kuwa Nyoso  aliwahi kuadhibiwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu. 

Nyoso amepewa adhabu ya kukosa mechi tano na faini ya Sh.milioni moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...