Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philipo Mpango amesema kuna baadhi ya watu nchini wamekuwa wakijidai wana shahada za uchumi lakini kiuhalisia ni mambumbu wa uchumi.
Pia amesema kutungwa kwa sera au kufanyika kwa maamuzi yasiyoendana na taaluma ya uchumi kunakopelekea kuumiza wananchi masikini kutokana na uwepo wa wachumi feki ambao wanapewa nafasi serikalini ,vyuoni hata kwenye sekta binafsi.
Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo na nyingine iko haja nchi kuwa na jJumuiya ya Wachumi au chama hai cha wachumi na chenye nguvu kwani ni muhimu sana.Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi chama cha Jumuiya ya Wachumi (EST) ambapo ametoa sababu tatu za umuhimu wa jumuiya hiyo.
Amefafanua sababu ya kwanza tasnia ya uchumi ina nafasi ya pekee katika kazi ya kujenga nchi kijamii,kiuchumi na hata kisiasa."Wachumi tunategemewa tuwe viongozi .Bila shaka waumini wenzangu wa John Maynard Keynes kuna maneno amewahi kuyasema na naomba nimnukuu.

Amesema hivi mawazo ya wachumi na wanafalsa wa siasa ,yawe sahihi au so sahihi yana nguvu kuliko inavyoeleweka kwa wengi."Watu wanaojiamini kwamba wako guru na ushawishi wa wanataaluma ,kiuhalisia watu hao ni watumwa wa mchumi fulani marehemu," amesema Dk.Mpango wakati ananukuu manneo ya Keynes.

Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji TIC na Mwenyekiti wa Kamati Uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wachumi Tanzania Economics Society Of Tanzania (EST) Bw. Godfrey Mwambe akipokea katiba ya Chama hicho kutoka kwa Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT)kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa jumuiya hiyo kwenye ukumbi wa BOT leo jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati anayeshuhudia ndiye aliyezinduam, Kulia ni Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati akizindua katiba ya chama hicho kwa kushirikiana na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakishiriki katika zoezi hilo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango katikati pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BOT)Profesa Florens Luoga na mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali wachumi wakionyesha katiba ya Jumuiya hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.

PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...