Na Karama Kenyunko, Globu  ya Jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema, Aprili 28 mwaka huu, itamsomea maelezo ya awali aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji uTanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano. 
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Tido, Ramadhani Maleta kuiomba Mahakama iwapatie muda wa kupitia maelezo ya awali ili aweze kushauriana na mteja wake kabla ya kusomwa. 
Kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Mhando kusomewa maelezo ya awali ambapo mwendesha mashtaka wa Takukuru Leonard Swai alidai wako tayari kumsomea. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo na wakili Maleta aliomba apewe muda kwa sababu alipatiwa maelezo hayo ya awali na upande wa mashtaka wakati wakiwa mahakamani hapo. 
Swai alipinga hoja hiyo na kudai kwa utaratibu wanapaswa kumsomea mshtakiwa maelezo hayo ya awali na Mahakama imuulize kipi anakubali na kipi anachokikataa na kwamba wanaweza kupitia kwa dakika tano. 
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano akiwa katika chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...