Na Said Nwishehe,Globu ya Jamii

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuna mambo mengi ya kujifunza na kubadilisha uzoefu kutoka kwa Majiji mbalimbali Barani Afrika kuliko majiji ya nchi za Ulaya.

Mwita amesema hayo leo, wakati akielezea ujio wa Meya wa Jiji la Blantyre nchini Malawi Wild Ndipo ambaye amekuja kwenye Jiji la Dar es Salaam akiambatana na viongozi wengine kwa lengo la kuja kubadilisha uzoefu kwenye nyanja mbalimbali.

Akizungumzia ujio wa Meya wa Jiji la Blantyre nchini Malawi,Mwita amesema kwenye mkutano wa mameya wa majiji mbalimbali ya Afrika uliofanyika nchini Afrika Kusini,walikubaliana kujenga utaratibu wa kutembeleana wao kwa wao.

Amesema kwa majiji ya Afrika kuna mambo ya kujifunza hasa kwa kuzingatia kuna mambo mengi yanafafana na hasa kwenye miundombinu ya barabara,elimu,afya na kilimo.Amefafanua kwa Majiji ya Ulaya mengi yamejengwa miaka 200 iliyopita na mingine zaidi hapo na kwa mazingira hayo hakuna cha kujifunza lakini kwa majiji ya Afrika kuna mengi ya kujifunza kwani hata umri wa majiji hayo unafafana.

Hivyo ujio wa Meya wa Malawi ni wa umuhimu zaidi kwani pamoja na mambo mengine watabadilisha uzoefu na kuweka mikakati ya kuboresha Majiji yao.Ameongeza Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Blantayre wameingia uhusiano wa urafiki kwenye lengo la kubadilisha mbibu na uzoefu kwenye mambo mbalimbali.

Mwita amesema ugeni huo ukiwa jijini Dar es Salaam watatembelea miradi ya maendeleo na kwa leo wamefanya mradi wa kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa lengo la kujifunza namna unavyoendeshwa.Kwa upande wa Ndipo ambaye ni Meya wa Jiji la Malawi amesema Jiji la Dar es Salaam kuna mengi ya kujifunza,hivyo wamepanga kutembelea maeneo mbalimbali ya mradi.

Pia amesema kubwa zaidi kesho watapata nafasi ya kushiriki kwenye kikao cha Baraza la Jiji,hivyo kuna kitu watajifunza.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza leo, ujio wa Meya wa Jiji la Blantaya nchini Malawi (kulia) ambaye amekuja kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali jijini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...